Skip to main content
Skip to main content

Waziri wa Utumishi wa Umma, Ruku afokea upinzani kuhusu bei ya mafuta

  • | Citizen TV
    366 views
    Duration: 1:44
    Waziri wa Utumishi wa Umma, Geoffrey Ruku, amewashutumu viongozi wa upinzani kwa kuikosoa serikali kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta huku akisema kuwa madai kuwa viongozi serikalini wanajinufaisha ni ya kupotosha. Akizungumza katika eneo la Mbooni wakati wa zoezi la ugawaji wa chakula cha msaada, Ruku amesema licha ya changamoto za kupanda kwa bei ya mafuta serikali ya kenya imeweka mikakati ya kuendelea kuwapunguzia makali wakenya. Aidha, aliwataka Wakenya kupuuza kauli za upinzani, akidai kuwa viongozi hao hawana mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazoikabili nchi.