Skip to main content
Skip to main content

Wetang'ula na Farouk wasema upinzani unaeneza chuki

  • | Citizen TV
    5,240 views
    Duration: 2:16
    Baadhi ya viongozi kutoka serikali jumuishi wakiongozwa na spika wa bunge la taifa Moses Wetangula na msaidizi wa rais Farouk Kibet wameendeleza kampeni ya kumpigia debe rais William Ruto ya mhula wa pili wakiusuta upinzani kwa kueneza siasa ya ukabila. Wakizungumuza huko Maturu eneo bunge la Lugari kaunti ya Kakamega, viongozi hao walimpongeza rais William Ruto kwa miradi ya maendeleo katika eneo pana la Magharibi na kurai jamii hiyo kuunga mkono uongozi wa Ruto. Aidha wamesema jamii hiyo inafaa kutwaa kiti cha urais baada ya uongozi wa Ruto.