- 4,265 viewsDuration: 2:12Zaidi ya watu 80 wameuawa na makundi ya watu wenye hasira katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki na Kusini kutokana na madai ya uongo kuhusu “Wizi wa nyeti” kwa wanaume, imebaini Idara ya BBC ya Kukabiliana na Taarifa Potofu Duniani. Mauaji hayo yanahusishwa na uvumi kwamba kuguswa tu begani kunaweza kusababisha sehemu za siri za mwanaume kusinyaa au kutoweka. Madai kama haya yanatokana na hofu na imani za kishirikina zilizodumu kwa muda mrefu na si jambo jipya barani Afrika, lakini mitandao ya kijamii imezidisha na kusambaza hofu hizi kwa kiwango kikubwa. Mwandishi wa BBC @alfredlasteck ameiangazia taarifa hiyo kwa kina. 🎥: @frankmavura #bbcswahili #tanzania #msumbiji Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw