
439 views
McCarthy awaonya Harambee Stars dhidi ya kuipuuzia Bafana Bafana
Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Harambee Stars, Benni McCarthy, amewaonya wachezaji wake kuwa Bafana Bafana watakuwa na ari ya kushinda wakati timu hizo zitakapokutana katika Uwanja wa Taifa wa Nyayo Jumanne usiku. Kocha huyo amesema kuwa baada ya sare ya mabao 2-2 Ijumaa usiku huko Soweto, Bafana Bafana haitaidharau Harambee Stars na itakuwa ikisaka ushindi katika mechi hiyo ya ugenini. Amewataka wachezaji wake kuwa na mtazamo sahihi, mawazo chanya na ari ya kupata matokeo mazuri. Mabadiliko kadhaa yatafanywa katika kikosi hicho, huku wachezaji wapya wakitarajiwa kupewa nafasi. Jack Vyner, anayecheza nchini Uingereza, hatimaye atapatikana kuichezea Kenya baada ya kupata pasipoti ya Kenya.
- Ruto awashutumu viongozi wa upinzani kwa kuchochea vijana kufanya fujo
- Tafakari Ya Babu: Mjinga na Mpumbavu
- Watu watano wauawa katika uvamizi wa wezi wa mifugo Isiolo
- “2024 Finance Bill was eventually passed, and there was no harm to our nation,” President Ruto says
- Amriya Super Cup yazinduliwa Mombasa kuwaepusha vijana na mihadarati wakati wa likizo
- Viongozi wa Kenya Kwanza Kitui washutumu upinzani kwa kuingilia uhuru wa IEBC
- Familia yaanzisha kilimo kando ya barabara Kangundo
- Wazazi Turbo wafurahia kufunguliwa tena kwa ufadhili wa basari za kaunti