
758 views
Gor Mahia yaizima Posta Rangers, KCB FC yapanda kileleni
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Gor Mahia wamerudia makali yao baada ya kuilaza Posta Rangers kwa mabao mawili kwa moja uwanjani Nyayo. Ushindi huo muhimu kwa K'Ogalo umepatikana kufuatia bao la dakika ya 81 lililofungwa na nahodha Alpha Chris Onyango. Gor walitangulia kwa bao la dakika ya 5 lililojibiwa dakika tatu baadaye na kisha mechi hiyo kuamuliwa dakika za majeruhi. Kwingineko, KCB FC wamerudi kileleni mwa ligi baada ya ushindi mwembamba wa moja bila dhidi ya 3K FC kwenye mchezo mwingine wa Ligi Kuu.
- Watu watano wauawa katika uvamizi wa wezi wa mifugo Isiolo
- “2024 Finance Bill was eventually passed, and there was no harm to our nation,” President Ruto says
- Amriya Super Cup yazinduliwa Mombasa kuwaepusha vijana na mihadarati wakati wa likizo
- Viongozi wa Kenya Kwanza Kitui washutumu upinzani kwa kuingilia uhuru wa IEBC
- Familia yaanzisha kilimo kando ya barabara Kangundo
- Wazazi Turbo wafurahia kufunguliwa tena kwa ufadhili wa basari za kaunti
- Gavana wa Kwale Fatuma Achani azindua shule mpya ya msingi Nalepo Mama Helena
- Viongozi Busia waonya kuhusu ongezeko la watoto wanaotelekezwa na wazazi