IMF yatoa wito kwa mataifa ya Kiafrika kuandaa miradi inayoweza kupata ufadhili

  • | VOA Swahili
    284 views
    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF, Kristalina Georgieva yuko nchini Rwanda kwa ziara ya siku tatu. Akiwa mjini Kigali amekutana na mawaziri wa fedha pamoja na magavana wa benki kuu za Rwanda, Uganda, Kenya na Sudan Kusini. Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kwamba shirika lake liko tayari kusaidia miradi mikubwa ya maendeleo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Amesema ili mataifa haya yaweze kufanikiwa kuna umuhimu wa kuandaa miradi mizuri ambayo inaweza kupata ufadhili hasa kwa kuzingatia kuwa pesa iliyopo haitoshi. #mkurugenzi #shirikalakimataifalafedha #imf #rwanda #afrikamashariki #voa #voaswahili #rwanda - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.