- 20,536 viewsDuration: 8:49Kifo cha kiongozi wa upinzani wa muda mrefu Raila Odinga kimeacha pengo kubwa la kisiasa nchini Kenya na kukiacha chama cha Orange Democratic Movement (ODM) na migawanyiko ya ndani. Katikati ya misukosuko hiyo, Katibu Mkuu wa ODM, na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ameonekana kuibuka kisiasa, akielezewa na wachambuzi kama “kimbunga cha kisiasa kinachochipuka” ambacho hakiwezi kupuuzwa. Lakini je, ataweza kuvaa viatu vya Raila Odinga? Na je, anataka kuwa rais wa Kenya?