- 17,580 viewsDuration: 5:49Bradley Marongo, anayefahamika na wengi kama Gen Z Goliath ana urefu wa futi 8.2, au mita 2.5, na ni mmoja kati ya wa watu warefu zaidi barani Afrika. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Kenya alijipatia umaarufu mkubwa baada ya kuonekana katika maandamano ya Gen Z mwaka 2024. Tangu wakati huo, Gen Z Goliath amekuwa mtengeneza maudhui mitandaoni, ameigiza sinema, na pia amekuwa balozi wa kampuni mbali mbali nchini Kenya. Lakini anakabiliwa na changamoto zipi kwa kuishi kama mtu mrefu hivyo? Mtangazaji Kinara wa Dira ya Dunia @roncliffeodit amezungumza naye katika studio za BBC Nairobi... #bbcswahili #mrefu #GenZ Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw