- 5,284 viewsDuration: 2:59Fred Obachi Machokaa ni mtangazaji nguli wa redio nchini Kenya. Mwezi huu anatimiza miaka 50 tangu aanze kazi kama mtangazaji wa redio. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni kumekuwa na dhana kwamba redio inapoteza umaarufu, hususan kutokana na ushindani mkali wa mitandao ya kijamii. Sasa swali ni je, redio imepitwa na wakati? Na je, ni nini ambacho lazima ufanye ili uwe mtangazaji bingwa wa redio? Mtangazaji Kinara wa BBC @RoncliffeOdit amemuuliza maswali hayo Fred Obachi Machokaa wakati akiadhimisha miaka 50 kama mtangazaji wa redio. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw