Vitisho vinavyozidi kuongezeka vya upotoshaji, taarifa za uwongo na kutiliwa chuku kwa maudhui ya mtandaoni ni masuala yaliyoangaziwa leo huku kongamano la sekta ya vyombo vya habari kuhusu umajumui wa Afrika la mwaka-2026 liking’oa nanga jijini Nairobi. Akihutubia wajumbe waliohudhuria hafla hiyo, katibu katika idara ya utangazaji na mawasiliano Stephen Isaboke alisema bara Afrika lazima lipige jeki haraka iwezekanavyo mifumo ya habari katika hatua ya kulinda demokrasia, imani ya umma na uadilifu katika enzi ya kidijitali.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive