- 40,169 viewsDuration: 2:24Bei ya mafuta Afrika Mashariki yazidi kupanda huku Kenya ikiongoza kwa gharama kubwa zaidi za dizeli na petroli ukanda huu. Wachambuzi wa uchumi wanasema zipo sababu kadhaa, lakini moja wapo ni kiwango cha kodi. Kwa mfano bei ya mafuta nchini Kenya inaongezwa na ushuru kadhaa na wa kiwango cha juu, ikiwa ni pamoja na gharama zingine za usambazaji wa ndani. Wakati Mataifa mengine kama Uganda na Ethiopia yanasemekana kuwa na mfumo tofauti wa kodi au ruzuku zinazosaidia kushusha bei ya mafuta kwa wananchi wao. Lakini je, Kwanini bei ya mafuta Uganda ni nafuu Kuliko Kenya na Tanzania? - - #bbcswahili #Mafuta #kenya #tanzania Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw