Skip to main content
Skip to main content

Maafisa kadhaa wa polisi wanusurika kifo Baringo baada ya gari lao kusombwa na mafuriko

  • | KBC Video
    503 views
    Duration: 2:19
    Kundi moja la maafisa wa usalama lililokuwa kwenye shughuli ya kiusalama lilinusurika kifo kwa tundu la sindano baada ygari lao aina ya Land Cruisa walimokuwa wakisafiria kusombwa na mafuriko ya ghafla kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika wadi ya Silale, eneo bunge la Tiati kaunti ya Baringo.Gari hilo lililokuwa likiwasafirisha maafisa wa polisi kwenda kuliokoa gari linguine la polisi lilikumbwa tatizo kama hilo baada ya kukwama kwenye matope katika mto Akwichatis wakati wa oparesheni hiyo ya uokoaji.hatahivyo magari yote mawili baadaye yaliondolewa kwenye matope.Viongozi wa sehemu hiyo wametoa wito kwa serikali iharakishe ujenzi wa barabara za usalama katika sehemu hiyo ili kuepusha matukio kama hayo. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive