- 6,507 viewsDuration: 2:04Furaha Chilambo, mkazi wa mkoa wa Mtwara kusini mwa Tanzania, amejifungua mapacha watano, uzazi adimu unaotokea mara chache duniani. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mimba za watoto wengi kwa wakati mmoja mara nyingi huhusishwa na matumizi ya tiba za uzazi kama dawa za kuongeza uwezo wa kupata ujauzito, teknolojia ya IVF au sababu za kurithi katika familia. Ili kufahamu hali yake na changamoto za kulea watoto hao, Mwandishi wa BBC @nyanza.halima amezungumza na mama wa watoto hao bi.Furaha Chilambo pamoja na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Afya ya Uzazi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini@szhmtwara , Dkt. Harry Mwambe, kuhusu sababu na athari za ujauzito wa aina hiyo. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw