- 32,611 viewsDuration: 1:18Raia mmoja wa marekani ashangaza kikao cha mahakama akidai kuwa chakula alichokuwa akipewa korokoroni hakimridhishi.Mmarekani huyo, Hodgkinson Enock Jedidah, ambaye anakabiliwa na shtaka la kuwa nchini kinyume na sheria asababisha kicheko katika mahakama ya Milimani akisema kuwa ugali na kabeji hazimfai na kumtaka hakimu mkuu mwandamizi kuagiza apewe chakula bora na cha kumtosha. Hata hivyo hakimu alimshauri kuridhika na chakula anachopewa. Mmarekani huyo alikanusha shtaka na kusema kuwa maafisa wa uhamiaji walitwaa stakabadhi zake za usafiri na kumfanya kushindwa kutafuta muda zaidi wa kuwa nchini. Mahakama iliagiza mshtakiwa huyoazuiliwe katika jela la Industrial area akisubiri maagizo zaidi.