- 8,989 viewsDuration: 3:12Mashirika ya usalama katika kaunti ya Kilifi yametangaza kukamatwa kwa mshukiwa mkuu anayehusishwa na unajisina mauaji ya kikatili ya Keziah Matuki wa umri wa miaka saba ambaye kifo chake kilizua ghadhabu za umma na maandamano miongoni mwa wakazi mapema juma hili. Mshukiwa huyo anayetarajiwa kufikishwa mahakama juma lijalo alikamatwa huku mamia ya wakazi wakiendelea kushinikiza haki kwa mtoto huyo wakati wa maandamano yaliyofanyika mjini Kilifi. Maafisa hata hivyo hawakubainisha maeneo kuhusu utambulisho wa mshukiwa huyo na mahala anakozuiliwa kutokana na sababu za kiusalama. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive