Skip to main content
Skip to main content

Mtoto wa miaka sita aweka rekodi ya kutatua Rubik’s Cub

  • | BBC Swahili
    5,972 views
    Duration: 30s
    Lian Yunzhi, mwenye umri wa miaka sita, ameweka rekodi mpya ya dunia kwa wanawake katika kutatua Rubik’s Cube yenye mistari 3 kwa kila upande baada ya kuivunja rekodi hiyo mara mbili ndani ya siku tatu. Kwanza alifikisha wastani wa sekunde 4.52, kabla ya kucheza tena hadi sekunde 4.27. Kwa matokeo hayo, amekuwa mwanamke pekee duniani mwenye wastani wa chini ya sekunde 4.5 katika mchezo huo. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Lian amekuwa akitumia takribani saa mbili hadi tatu kila siku kufanya mazoezi ya mbinu za kutatua Rubik’s Cube. #bbcswahili #china #RubikCube Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw