Skip to main content
Skip to main content

Mvulana aokolewa akiwa hai katika jengo lililoporomoka Gaza

  • | BBC Swahili
    2,398 views
    Duration: 29s
    Mvulana mwenye umri wa miaka minne ameokolewa akiwa hai kutoka kwenye vifusi baada ya jengo la ghorofa sita kuporomoka katika Mji wa Gaza. Mtoto huyo, ambaye alikuwa amejeruhiwa vibaya, alikutwa akiwa amelala pembeni ya mwili wa mama yake aliyefariki. Takribani watu wengine 21, wakiwemo watoto wanane, walifariki baada ya jengo hilo lililoharibiwa na vita kuporomoka wakati wa usiku. Jengo hilo lilikuwa tayari limeharibiwa na vita na lilikuwa limeegemea upande, lakini baadhi ya familia zilizokuwa zimepoteza makazi ziliendelea kuishi humo kwa sababu hazikuwa na makazi mbadala. #bbcswahili #gaza #palestine Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw