- 13,295 viewsDuration: 1:58Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Thaddaeus Ruwa’ichi, amesema Tanzania kwa sasa haijajengwa katika misingi ya uadilifu, kauli inayozua mjadala kuhusu umuhimu wa haki, uaminifu na maadili katika uongozi na maisha ya jamii. Akizungumza leo, Askofu Mkuu Ruwa’ichi pia ameeleza kuwa Kanisa Katoliki linaendelea na mchakato wa kumtangaza Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa mwenye Heri ndani ya Kanisa Katoliki. Mwalimu Nyerere, aliyefariki mwaka 1999, anakumbukwa kwa msisitizo wake kuhusu uadilifu, usawa, utu na uwajibikaji katika uongozi. #bbcswahili #tanzaniatiktok #nyerereday Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw