- 2,630 viewsDuration: 4:14Kenya imemtambulisha rasmi mgombea wake wa nafasi kwenye jopo la majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, huku Rais William Ruto akitafuta uungwaji mkono wa kimataifa kwa jaji wa Mahakama ya upeo Njoki Ndung’u. Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi, Rais aliutaja uwaniaji huo kuwa msukumo wa kuimarisha haki, uaminifu, na uwakilishi wa Afrika katika haki za kimataifa. Uteuzi huo sasa unaweka msingi wa kampeni ya kidiplomasia kabla ya uchaguzi wa mahakama hiyo kwa mihula ya 2027-2036. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive