Skip to main content
Skip to main content

Roketi ya spaceX Starship yalipuka baada ya safari ya angani

  • | BBC Swahili
    7,295 views
    Duration: 36s
    Roketi ya SpaceX aina ya Starship imelipuka baada ya kutua katika Bahari ya Pasifiki ikirejea kutoka angani. Kwa sasa, sababu ya mlipuko huo haijajulikana. Roketi hiyo ilipangwa kufanya safari ya takribani saa kumi, lakini iliamuliwa irudi mapema baada ya kuzunguka Dunia kwa muda wa saa tatu. Wakati wa safari hiyo, Starship ilifanikiwa kupeleka satelaiti 26 za Starlink V3 za kizazi kipya, ambazo zimeongezwa kwenye mtandao wa satelaiti za Starlink unaotoa huduma ya intaneti ya kasi kwa maeneo mbalimbali duniani. #bbcswahili #starlink #teknolojia #angazajuu #roketi #spaceX Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw