Naibu Rais Kithure Kindiki amewahakikishia wakazi wa kaunti ya Kitui kuwa serikali imeimarisha usalama kufuatia mauaji yaliyotokea katika maeneo ya Tseikuru na Kathungu. Haya yanajiri baada ya watu saba kuuawa na watu wanaodaiwa kuwa wafugaji wa ngamia, na wengine wanane kuuawa kwenye mashambulizi ya kulipiza kisasi katika mzozo kwenye mpaka wa Garissa na Kitui. Aidha, mwanafunzi wa gredi ya saba aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye makali katika eneo la Kathungu, Kitui, tukio linalodaiwa kuhusisha wafugaji hao wa ngamia.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive