Wakazi wa Mji wa Embu na maeneo jirani wameeleza wasiwasi kutokana na ongezeko la wizi, uvamizi na uporaji.
Wakazi hao wanataka hatua za haraka za kiusalama kuchukuliwa, Wakilalamikia kuhangaishwa na magenge ya wahalifu haswa usiku. nyakati za usiku.Baadhi ya wakazi wameripoti kupoteza magari yao katika mazingira ya kutatanisha.
Wafanyabiashara pia wameonya kuwa hali hiyo inaweza kuathiri uchumi wa eneo hilo, huku uongozi wa kaunti ukithibitisha kuitisha kikao cha dharura cha usalama ili kushughulikia tatizo hilo.