Kabila kuvuliwa kinga ya Urais

  • | BBC Swahili
    50,322 views
    Bunge la Seneti la DRC limeondoa kinga ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila, na hivyo kumtengenezea njia ya kufunguliwa mashitaka. Kwa jumla, Maseneta 88 walipiga kura ya kuunga mkono kuondolewa kwake kwa kinga hiyo ili aweze kushtakiwa, ni watano pekee waliopiga kura kupinga hilo, huku kura nyingine tatu zikiharibika. Anakuwa mkuu wa nchi wa kwanza wa zamani kuondolewa kinga hiyo na kushtakiwa kwa uhaini, uhalifu wa kivita na mashtaka yanayohusiana nayo nchini DRC. Mwandishi wa BBC @mubalileonard anasimulia 🎥@bosha_nyanje - - #bbcswahili #DRC #Kabila #viongozi #rais Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw