- 5,068 viewsDuration: 1:32Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi tume huru ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu mwezi uliopita nchini humo. Rais Suluhu ameitaka tume hiyo kuchunguza kiini cha machafuko yaliyoshuhudiwa pamoja na matamshi ya wanachama wa upinzani tanzania. Rais Samia pia ameagiza mashirika yasiyo ya serikali kuchunguzwa kwa mchango wao hasa katika ufadhili wa machafuko nchini Tanzania.