Skip to main content
Skip to main content

Ruto atangaza hazina mpya za miundombinu na utajiri wa rasilimali kufadhili miradi ya maendeleo

  • | Citizen TV
    1,629 views
    Duration: 3:57
    Je, Miradi inayotazamiwa na Rais William Ruto kulitoa taifa kutoka kwenye hadi ya taifa linalostawi hadi taifa lililostawi itafadhiliwa vipi? Kwenye hotuba yake bungeni, rais Ruto ametangaza kuzinduliwa kwa Hazina ya Kitaifa ya Miundombinu na Hazina ya Utajiri wa Raslimali ya Nchi. Kwa mujibu wa rais, Hazina hizo zitapunguza haja ya kukopa pesa katika nchi za kigeni au kuwaongezea wananchi mzigo wa ushuru. Rais Amesema kwamba Mapato yote yatakayopatikana kufuatia ubinafsishaji wa baadhi ya mashirika ya Serikali yataelekezwa kwenye hazina ya miundombinu, ambayo itatumika kuvutia faida ya hadi mara 10 zaidi ya sasa. Rais anasema kuwa Mfuko wa Utajiri wa Raslimali ya nchi utaokoa sehemu ya mapato ya rasilimali kwa vizazi vijavyo