Skip to main content
Skip to main content

Mwanafunzi wa gredi ya 10 alipiwa karo na vifaa

  • | Citizen TV
    1,488 views
    Duration: 2:42
    Machozi ya furaha yalimbubujika baada ya wasamaria wema kujitokeza kumsaidia Elias Mwangi, mwanafunzi ambaye aliangaziwa akitembea mitaa ya mji wa Nanyuki akitafuta msaada wa karo ya shule. Elias, mwanafunzi kutoka mtaa wa Likii katika Kaunti ya Laikipia, alikuwa ameacha ndoto yake ya kuanza masomo ya secondari ya juu ya gredi ya 10 kutokana na ukosefu wa karo. Elias Mwangi: (I am greatful that l will no longer go to sleep hungry, i'll be drinking tea and my uniform is already taken care of. I'm really happy.) Elias alipata alama 66 katika mtihani wa gredi ya 9, lakini hata hivyo hakufaulu kuripoti shuleni kwa kukosa karo. Mamake, ambaye anaripotiwa kukumbwa na changamoto ya uraibu wa pombe, hakuweza kumudu mahitaji ya familia. Susan Muthoni: ( Nilikuwa nimeshindwa kumsomesha juu ya ile kazi nilikuwa nafanya ilikuwa illegal, wakati niliacha kupika kitu nilikuwa napika nikashindwa kumsomesha.) Jessee Maina: (I wish him well, aende asome vizuri, aaona ile shida tulipitia ya kuzunguka tukitafuta usaidizi na mtu yoyote amesaidia Asante sana.) Hatimaye, msaada ulipatikana kupitia shirika la Golden Greens, ambalo limesema litagharamia masomo yake yote kwa kipindi chote cha miaka mitatu ya shule ya sekondari ya juu, ikiwemo sare za shule, vifaa vya masomo na mahitaji mengine muhimu. Bernard (Tutamaomesha all the years atakuwa hapa. Tumeanza na first term, tumemake sure tumelipa school fees and we've made the commitment kumsomesha throughout his senior school life.) Susan Wanjiru: (i'll be able to mentor him kama mzazi na kufuatilia masomo yake nione ya kwamba anaendelea vizuri jinsi vile mtoto anapaswa kuwa anasoma na kufuatilia kwa karibu.) Kwa sasa, Elias Mwangi ana sababu ya kutabasamu. Ndoto yake ya kupata elimu na kuwa mhandisi wa ujenzi imepata uhai mpya.