Chama cha madaktari- KMPDU tawi la Nairobi, kimesitisha mgomo wao kwa muda wa siku thelathini, na kuashiria mwisho wa mgomo wa siku 45 uliolemaza huduma za afya ya jijini Nairobi. Wakizungumza leo katika hospitali ya Mbagathi, viongozi wa chama hicho walisema wamechukua hatua hiyo kufuatia agizo la mahakama, la kuwataka madaktari na serikali ya kaunti ya Nairobi kuafikia makubaliano ya kurejea kazini. Na kama mwanahabari wetu John Kahiro anavyoripoti,madaktari wamesisitiza kwamba, iwapo serikali ya kaunti itashindwa kushughulikia malalamiko yao, basi hawatakuwa nabudi ila kurejelea mgomo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive