Waasi warepotiwa kuua mama, mtoto na kuteka wauguzi DRC

  • | VOA Swahili
    2,134 views
    Watu wenye silaha wavamia hospitali muhimu ya Kabasha, malori na maduka ya wananchi nyakati za usiku na kumuua mama moja na mtoto mchanga kwa kuwapiga risasi. Pia watu hao wanaodhaniwa kuwa waasi wa ADF waliwateka wauguzi wawili wa kituo cha afya na wakaazi wengine zaidi ya kumi ambao hawajulikani waliko. Sikiliza repoti kamili kuhusu hatua inayochukuliwa na jeshi la DRC likishirikiana na jeshi la wananchi wa Uganda... - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.