Daktari bandia Mugo wa Wairimu ahukumiwa miaka 29 jela

  • | Citizen TV
    563 views

    Daktari bandia Mugo wa Wairimu atatumikia kifungo cha miaka 29 na miezi sita. Wairimu alipatikana na makosa kumi ya kutumia dawa za kupambaza kwa madhumuni ya kuwabaka wateja wake na pia kuhudumu bila leseni. Hakimu Wendy Muchemi amesema kuwa Wairimu ni tishio kwa jamii na anastahili kuwa mbali na umma. Hakimu Wendy amesema kuwa Wairimu alitumia vibaya ujuzi wake wa udaktari ili kuwadhulumu wanawake badala ya kutumia ujuzi huo kwa manufaa ya jamii. Awali Wairimu aliitaka mahakama kumruhusu kuhudumia taifa na kutimiza ndoto zake za udaktari