Mmiliki wa jumba lililoporomoka Ruaka akamatwa

  • | Citizen TV
    3,418 views

    Mmiliki wa jumba lililoporomoka na kuwaua watu wawili eneo la Ruaka juma lililopita amekamatwa. Mshukiwa aliyekuwa akitafutwa tangu tukio hilo alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta akijaribu kuondoka nchini. Kamishna wa kaunti ya Kiambu Joshua Nkanatha akisema kuwa mtu huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kiambu akisubiri kufikishwa kortini. Jumba hilo liliporomoka na kusababisha vifo vya mtu na mkewe. kwa mujibu wa Nkanatha, mmiliki huyu pamoja na wahusika wengine wakiwemo maaafisa wa kaunti na wahandisi huenda wakashtakiwa. Kukamatwa kwake kukijiri saa chache baada ya jumba jingine kuporomoka katika eneo la Ruiru kaunti hiyo hiyo ya Kiambu