Watahiniwa 248 wana ujauzito kaunti ya Narok

  • | Citizen TV
    284 views

    Haya yakijiri, zaidi ya wanafunzi mia mbili kaunti ya Narok wamefanya mitihani yao ya gredi ya sita na darasa la nane wakiwa waja wazito. Wanafunzi hawa 248 wakiwa miongoni mwa jumla ya wanafunzi elfu 69 waliofanya mitihani hii kaunti ya Narok. Kamishna wa kaunti ya Narok Isaac Masinde aliyeongoza zoezi la kufungua kontena za mitihani kaunti hii ametoa hakikisho kuwa wanafunzi hao watapokea mazingira bora ya kiafya hata wanapofanya mitihani yao. Kaunti ya Narok imekuwa ikiongoza kwa idadi ya wasichana wanaowacha shule kutokana na mimba za mapema, kulingana na ripoti ya mwaka huu ya wizara ya elimu nchini