- 94 viewsDuration: 1:45Zaidi ya watoto 6000 wa kike katika wadi ya Jilore, eneo bunge la Malindi wamenufaika na msaada wa Sodo zinazoweza kuoshwa baada ya kutumika. Wafadhili wa mpango huo chini ya shirika la Watoto Kenya wamesema usaidizi huo unawalenga watoto wanaotoka familia maskini katika eneo hilo. Aidha mpango huu pia unahusisha kuwapa zaidi ya wanafunzi 2000 chakula cha mchana ili kuwasaidia kusalia shuleni na kuimarisha elimu katika eneo hilo. Wazazi wamepongeza mpango huo wakisema utasaidia kuhakikisha watoto wanasalia madarasani hasa baada ya kushuhudiwa kwa kiangazi Kwa muda mrefu.