- 106 viewsDuration: 1:46Ni afueni kwa waathiriwa wa dhuluma za kijinsia baada ya serikali ya kaunti ya Tana River pamoja na mashirika ya kijamii kuzindua sera itakayotoa mwongozo wa jinsi waathiriwa wa dhulma hizo watakavyo shughulikiwa kisheria. Akizindua sera hiyo mjini Hola, Waziri wa jinsia katika kaunti ya Tana River Abass Kunyo alisema sera itahakikisha kuwepo kwa kituo cha kuwasaidia manusura wa dhulma za kinjisia na wahusika kukabiliwa vilivyo kisheria. Aidha sera hii inatarajiwa kushinikiza bunge la kaunti hiyo kutenga fedha za kufanikisha ajenda hiyo.