Familia moja kutoka eneo la Kiunga kaunti ya Lamu inatafuta majibu kuhusiana na kutoweka kwa mvuvi aliyetekwa nyara na wanaume zaidi ya Sita ambao waliokuwa wameficha nyuso zao wiki iliyopita.
Mohammed Omar, mwenye umri wa miaka 41, alitekwa nyara tarehe 12 Septemba nyumbani kwake. Familia yake inasema wamesema kuwa licha ya kutafuta habari kutoka kwa polisi, hawajapata jibu. Aidha Shirika la Haki Africa linamtaka inspekta jenerali wa polisi kutoa taarifa rasmi kuhusu kutoweka kwa Mohamed na iwapo waliomteka ni polisi au la.