Wauguzi Kisii wametangaza mgomo

  • | Citizen TV
    390 views

    Kwa mara nyingine muungano wa wauguzi KNUN kaunti ya Kisii umetangaza mgomo wa kushinikiza serikali ya kaunti hiyo kutekeleza ahadi iliyotoa kwao. Miongoni mwa ahadi hizo ni kuwapa wauguzi barua za kuajiriwa, kuwapandisha vyeo na kuboresha mazingira ya kazi. Wakihutubia wanahahabari mjini Kisii, viongozi wa muungano huo wametaka waziri wa afya kutimiza ahadi zilizotolewa kwa wahudumu hao wa afya.cHata hivyo akizungumza na runinga ya Citizen kwa njia ya simu waziri wa Afya kaunti ya Kisii, Ronald Nyakweba amesema kuwa tayari barua zinaendelea kuandikwa akiwataka wauguzi wawe na subra serikali ikiwa mbioni kutekeleza ahadi hiyo.