
171,803 views
9 May 2025
Lyrics *CHUO NIKIPENDACHO* *1Chuo nikipendacho japo ni cha zamani kinanikumbusha mambo ya kale wakati wa utoto nilikuwa kwa mama naye akasomea chuo hicho* *Kitabu nikipendacho Bibilia takatifu Maneno matamu mazuri ya uzima, Mwanzo Ufunuo mwisho maktaba halisi* *2.Alikisoma chuo nazo hadithi zake Kuhusu watu wa kale watu wa Mungu Yusufu na Danieli Daudi na GolayaHadithi zao zatufunza kumtii Mungu* *3.Akasoma kuhusu Yesu mwenye upendo Vile alivyokufa msalabani Nikiwa na huzuni alinibembeleza Akanibusu kwa upendo mwingi* *4. Ni mambo ya zamani bali nayakumbuka Maneno ya chuo hiki nikipendacho Napenda kuyatii kama nilivyofunzwa Yamebaki katika moyo wangu*
