
1,040 views
Watunza Misingi feat Kella B, Tinie Cousin, Kido Boma and Ras Muhemsi
19 Feb 2022
#SiBe #watunzamisingi 2022 WIMBO WA TATU KUACHIWA TOKA KWENYE ALBUM YA SI.BE ALBUM INAPATIKANA KWA MFUMO WA HARDCOPY(CD) na SOFTCOPY(EMAIL/WHATSAP/TELEGRAM) https://linktr.ee/watunzamisingi VERSE 1: KELLA B Nipo zangu ndani nimejipumzikia Kuna kelele nje Ikanishtua Nikanyanyuka dirishani nikasogeza kidogo pazia Kuchungulia nje kuangalia kinachoendelea Ni kelele za raia kupinga kuendelea kuonewa Matatizo yao kutotatuliwa Wamama wanalia Mwanao kabakwa na mtoto wa kigogo na hakuna hatua anayochukuliwa Watu jazba juu Wanasema Haiwezekani usawa huu Nikasikia Haya mambo hadi lini, nikajua hapa pana makuu Watu wamechachamaa, haidhurumiwi haki ya mtuu Muda huu Wataijua kiu yetu Wamejisahau wanaona poa kwao kilasiku kuwa sikukuu Tumechoka kusubiri chini tunawapandia hukohuko tupate suluhu Hii nchi ni yetu sote kuna watu wamejisahau Kwanini Wanafanya wanachojiamlia Hawafuati katiba wala sheria Yani mwenye nafasi akizingua ishu yake wanaipotezea Don't fool all the poople all the time muda umewadia Kuna mambo kibao, hamkawii kusema hiyo sasa bangi Nadhani kuweka wazi ni jambo la msingi Kama mgao wa umeme masaki ndio kunatakiwa ukatwe masaa mengi Uswahilini hakuna majenereta ni choka hakuna ma kingi
