
4,605 views
St. Anthony Cathedral Choir Malindi
4 Jun 2026
Mazingira (Vol. 5) 1. Mazingira ni uhai, mazingira ni uzima, ni wajibu wetu sote tuyatunze mazingira x2 [Baba mama hata watoto, pamoja twendeni sasa; Asikofu na makasisi watawa na waumini; {Tupande miti kwa wingi, Tukuze miti kwa wingi, tupate maji hewa safi kivuli na matunda} x2] x2 2. Mazingira ni makao, nyumbani kwa viumbe vyote, Wanyama samaki ndege binadamu na wadudu x2 3. Tusitupe takataka, ndani ya bahari kamwe, tusikate miti wala tusifunge mito kamwe x2 4. Mazingira ni rafiki, rafiki mpendwa wetu, tukiyaharibu leo yatatuharibu kesho x2 COPY RIGHT BY ST ANTHONY CATHEDRAL CHOIR MALINDI
