
10,550 views
St. Anthony Cathedral Choir Malindi
26 Mar 2026
NI KOSA GANI HILO? 1. Taji la miiba kichwani mijeledi na mateso makali yaliyompata Yesu, hadi mlimani, uchungu mwingi, huzuni tele, wauaji kwa hasira bila huruma wanasema.. (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Mpe siki na sio maji' - (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Heri mwizi kuliko Yesu' - (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Jiokoe mwenyewe sasa' - (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) 2. Dhambi zetu nyingi ni sehemu ya uzito wa msalaba ulio mwangusha Yesu chini mara tatu, maneno yetu, matendo yetu ni sawa na Mayahudi walio piga makelele... (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Hata pasipo makosa tu' - (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Hakujibu hata neno tu' - (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Hawanui walitendalo' - (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) 3. Makuhani hata na Mafarisayo wanaishi na bado wanamkana mwokozi siku hadi siku, ni ndugu zetu, rafiki zetu, anasa ushirikina ni kama ule msalaba... (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Yuda bado ni msaliti' - (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Hatujui tulitendalo' - (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Tumemwacha muumba wetu'- (Auawe, inabidi auawe atundikwe msalabani) Climax: Tenor & Bass: Pilato akasema, mimi sioni kosa kwake, mchukueni ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa sheria ya kiyahudi,) Oh' alisema (kwamba) yeye ni mwana wa Mungu, (tena) atalibomoa hekalu hili lililojengwa miaka mingi, na kulijenga kwa siku tatu, nikosa gani hilo, lisilo na msamaha, alilofanya mwokozi Yesu Kristo hadi kufa msalabani? COPY RIGHT ST ANTHONY CATHEDRAL CHOIR MALINDI
