Skip to main content
Skip to main content

Afueni ya karo

  • | Citizen TV
    839 views
    Duration: 1:59
    Familia moja jijini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu ambayo ilikuwa imeshindwa kuwapeleka watoto wao wanane shuleni sasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kupata ufadhili wa masomo. Wanafunzi hao sasa wameweza kuanza masomo baada ya naibu spika Gladys Boss kuwalipia karo wote.Familia hiyo ilikuwa imepewa barua kutoka kwa chifu wa eneo hilo ili waweze kuomba msaada kutoka kwa wakenya. Runinga ya Citizen iliangazia masaibu yao na mahangaiko ya kutafuta karo ili waweze kwenda shule lakini sasa wote wanane wamepata fursa ya kuafikia ndoto zao.