- 802 viewsDuration: 3:15Kampuni za mawasiliano ya simu zimewekwa kwenye darubini baada ya ripoti ya shirika la amnesty international kuzihusisha na madai ya kusakwa kwa wanaharakati wakati wa maandamano ya mwaka 2024–2025. Katika ripoti yake amnesty inaishutumu serikali ya kenya kwa kutumia teknolojia kuwasaka, kuwakamata na kuwatisha waandamanaji, ikidai kuwa kampuni hizo ziliwezesha upatikanaji wa data za simu zilizotumiwa na vyombo vya usalama.