Asilimia 95 ya eneo lote lililofanyiwa uchimbaji wa madini na kampuni ya Base Titanium katika kaunti ya Kwale limefanyiwa marekebisho na kurejeshwa hali yake ya kawaida baada ya shughuli za uchimbaji kukamilika Disemba mwaka wa 2024.
Takriban miti 300,000 na nyasi za kiasili tayari zimepandwa katika ardhi hiyo ya ekari zaidi ya 4,000 na sasa iko katikauangalizi wa kitaalam kabla ya mashamba hayo kutumika tena kama itakavyoelekezwa na serikali.
Aidha bwawa la Mkurumudzi lililokuwa likitumika kwa shughuli za uchimbaji madini limewekwa mikononi mwa halmashauri ya maji ya pwani ili kuanza kuwasambazia wananchi maji safi.