Baadhi ya wabunge na maseneta wamependekeza kuongezwa kwa mgao wa bajeti ya wizara ya kilimo na mifugo ili kuimarisha sekta hiyo na kuzuia taifa dhidi ya kuagiza chakula kutoka nje ya nchi.
Wakizungumza baada ya kukutana na wasimamizi wa mashirika ya serikali na maafisa wa wizara mjini Malindi, mwenyekiti wa kamati ya kilimo na mifugo katika Bunge la Kitaifa Dkt John Mutunga na seneta wa kuteuliwa wa kamati ya Seneti ya kilimo, mifugo na uvuvi Hezena Lemaletian wamedokeza kuwa , ili Kenya iwe na utoshelevu wa chakula, sekta hiyo inahitaji ufadhili wa pesa zaidi.