CCM yasema Martha Karua wa Kenya alingilia maamuzi ya mahakama

  • | BBC Swahili
    118,670 views
    Chama tawala nchini Tanzania CCM kimesema suala la mwanasiasa wa Kenya Martha Karua kuingilia maamuzi ya mahakama ya nchi hiyo ndio lililosababisha kuzuiliwa kwa wanaharakati wengine waliotaka kuja kushuhudia kesi ya mwanasiasa wa upinzani Tundu Lissu. Katika mahojiano maalum na BBC, Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Stephen Wasira amesema hatua hiyo ilikua ni kama kuingilia maamuzi ya ndani ya nchi kitu ambacho hakikubaliki. Ameanza kwa kumuelezea mwandishi wa BBC David Nkya malalamiko ya kwamba vyombo vya dona nchini humo vinatumika kuukandamiza upinzani. #bbcswahili #tanzania #ccm Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw