Skip to main content
Skip to main content

Chaguzi Ndogo ya Ol Kalou I Vyama vya kisiasa vyashtumiwa kwa kukiuka kanuni za IEBC

  • | KBC Video
    524 views
    Duration: 2:08
    CHAGUZI NDOGO OL KALOU Kamati ya usalama ya kaunti ya Nyandarua imedai kwamba vyama vya kisiasa vinavyowania uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Ol Kalou, vinakiuka kanuni za Tume Huru ya Uchaguzi na Uratibu wa Mipaka (IEBC) kuhusu saa za kampeni. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdirisack Jaldesa, ambaye pia ni Kamishna wa Kaunti ya Nyandarua, aliwahimiza wagombea kuhakikisha wafuasi wao wanahitimisha mikutano yao kabla ya usiku kuwadia ili kudumisha usalama na utulivu wa umma. Akizungumza afisini mwake, Jaldesa alielezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la visa vya vurugu na uharibifu wa vifaa vya kampeni. Pia aliwashauri wagombea wote kuwajulisha polisi mapema kuhusu shughuli zao za kampeni ili kuweka mipango kabambe ya usalama. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive