Waziri wa Afya, Adan Duale, amesema kuwa serikali italipa shilingi bilioni nne inazodaiwa na vituo vya afya kufikia wiki ijayo.
Duale anasema kuwa madeni hayo yaliyokuwa ya NHIF yamejumuishwa katika bajeti ya ziada.Hospitali ambazo zinadai chini ya shilingi milioni kumi ndizo zitakazolipwa kwanza. Duale anasema hatua hiyo itasaidia vituo vidogo vilivyoathirika zaidi kifedha. Madeni yaliyosalia yatahakikiwa na kujumuishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2026 hadi 2027, na malipo yake kuanza mwezi kulipwa Julai.Vituo vya afya vya umma,kibinafsi na vya kidini vinakabiliwa na changamoto kubwa za kifedha kutokana na kutolipwa kwa huduma walizotoa chini ya NHIF.