- 1,229 viewsDuration: 1:09Waziri wa afya Aden Duale amerejelea wito wa kufunguliwa kwa mpaka wa Kenya na Somalia akisema serikali inaendele kupoteza mapato mengi kupitia biashara za magendo zinazofanyika kwa njia ya mkato. Akizungumza mjini Garissa Duale amesema kufunguliwa kwa mipaka hiyo kutainua uchumi katika kaunti za Kaskazini Mashariki na kupunguza ugumu wa kuhakiki uhalisi wa raia wa nchi jirani kupitia kituo cha forodha.