Elimu Bora lataka uteuzi wa sekondari usitishwe hadi kasoro za KCPE zishughulikiwe

  • | Citizen TV
    476 views

    Shirika la Elimu Bora limeelekea mahakamani kutaka shughuli ya uteuzi wa wanafunzi wa sekondari kusitishwa hadi kasoro za KCPE zishughulikiwe. Kulingana nao kulikuwa na utepetevu miongoni mwa maafisa wakuu wa elimu nchini hali iliyosababisha kuwepo kwa dosari katika mtihani huo ambao ulikuwa wa mwisho nchini. Elimu Bora wanasema kuwa haki za kimsingi za wanafunzi zilikiukwa na kukosoa baraza la mtihani nchini KNEC kwa kutokuwa wazi kuhsu namna makosa yalitokea na yatakavyorekebishwa