- 8,811 viewsDuration: 3:48Eneo bunge la Lamu Mashariki ambalo ni eneo la Visiwa limepata barabara ya kwanza ya Lami tangu Kenya kupata Uhuru. Barabara hiyo inayoendelea kujengwa Kisiwa cha Pate itarahisisha usafiri na kupunguza hasara wanayopata ya kusafirisha mizigo na binadamu. Barabara ya sasa imejaa mashimo na kuwa na matope wakati mvua inaponyesha, hali inayosababisha gharama ya usafiri kuongezeka.