Familia moja inaomboleza vifo vya jamaa 6 waliofariki jana kwenye ajali Laikipia

  • | Citizen TV
    7,056 views

    Familia moja katika kijiji cha Tesi kaunti ya Laikipia inaomboleza vifo vya jamaa sita waliofariki kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea barabara kuu Ya Nyeri-Nyahururu jana jioni. Ajali hiyo ilihusisha matatu, gari la binafsi na pikipiki na kusababisha jumla ya vifo 9. Ni ajali ambayo imepandisha idadi ya watu walioaga barabarani kufikia 17 wiki hii pekee.